Biden asema Marekani ilimuua kiongozi wa al-Qaida katika shambulizi la droni huko Afghanistan
2022-08-02 09:42:48| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza kuwa kiongozi wa kundi la al-Qaeda Ayman al-Zawahiri ameuawa katika shambulizi la droni mjini Kabul, Afghamistan, na kuongeza kuwa hakukuwa na majeruhi ya raia.

Al-Zawahiri aliteuliwa Juni 2011 kumrithi Osama bin Laden kama kiongozi wa al-Qaida, mwezi mmoja baada ya bin Laden kupigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wa Marekani huko Abbottabad, Pakistan.