Msemaji: Tsai Ing-wen na mamlaka za DPP kuiingiza Taiwan kwenye majanga makubwa kwa kushirikiana na makundi ya nje
2022-08-04 11:11:01| CRI

Msemaji wa Ofisi inayoshughulikia masuala ya Taiwan ya Baraza la serikali ya China Ma Xiaoguang, amesema jaribio la kiongozi wa Taiwan, Tsai Ing-wen na mamlaka za Chama cha Maendeleo ya Demokrasia (DPP) la kushirikiana na makundi ya nje litaiingiza Taiwan kwenye majanga makubwa.

Ameeleza kuwa Tsai na mamlaka za DPP wameshikilia msimamo wa ufarakanishaji wa “kuifanya Taiwan ijitenge na China” na kukataa kutambua makubaliano ya mwaka 1992, kuhamasisha waziwazi utetezi wao wa “mataifa mawili” na kushambulia sera ya “nchi moja, mifumo miwili”.

Kwa mujibu wa Ma wamesababisha kwa makusudi makabiliano kwenye mlango bahari wa Taiwan, kuteka maoni ya watu wa kisiwani, kusikiliza watu wenye maoni ya ouvu kwenye jamii ya watu wa Taiwan na kufanya kila juhudi za kukandamiza makundi ya watu waadilifu na sauti za busara ambazo zinaunga mkono maendeleo ya amani ya uhusiano wa mlango bahari na kuungana tena kwa amani.

Wakati huohuo Kamandi ya Uwanja wa Vita wa Mashariki ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) imeandaa mazoezi ya kijeshi katika maeneo ya baharini ya pwani ya kaskazini, kusinimagharibi na kusinimashariki mwa kisiwa hicho na anga zake. Mazoezi hayo yanashirikisha vikosi vya askari maji, wa anga, wa roketi, vinavyounga mkono kimkakati na vya ugavi.