China kuchukua hatua thabiti, za nguvu na zenye ufanisi ili kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa China
2022-08-04 11:11:37| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema hatua za China dhidi ya ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi kisiwani Taiwan, zitakuwa thabiti, za nguvu, na zenye ufanisi.

Akijibu swali kuhusu China kuchukua hatua zote za lazima ili kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa China, Bw. Hua amewaambia wanahabari kuwa matokeo yote yatakayojitokeza yatabebwa na Marekani na makundi ya ufarakanishaji ya kuitaka “Taiwan ijitenge na China”.

Amesisitiza kuwa chokochoko zote za Marekani wanazoifanyia China mwisho huwa wanajiabisha wao wenyewe, na kutolea mfano wa tukio la hivi karibuni, ambapo Pelosi na watu wengine walichochea vurugu huko Hong Kong na kutetea eti kile kinachoitwa “mazingira mazuri”, lakini matokeo yake waliongeza kasi ya mageuzi ya Hong Kong ya kuiondoa kwenye vurugu na kuiingiza kwenye utulivu na ustawi na kuifanya ing’are tena.