Rais Mnangagwa asema Zimbabwe itastawi licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi
2022-08-04 11:12:51| CRI

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapa kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Zimbabwe, akionya kwamba nchi za Magharibi ambazo zimeiwekea vikwazo nchi hiyo hazitafanikiwa katika njama zao za kuivuruga nchi hiyo.

Alisema Zimbabwe itafikia matarajio yake ya maendeleo licha ya vita vya kiuchumi vinavyoendeshwa dhidi ya nchi hiyo na mkoloni wa zamani Uingereza na washirika wake.

Alisema vikwazo vilivyowekwa kwa zaidi ya miaka 20 na nchi za Magharibi, ambavyo vilikusudiwa kudhoofisha uchumi wa Zimbabwe, na kuwalazimisha raia kujitokeza kupambana na serikali iliyopo madarakani ya ZANU-PF, hadi sasa vimeshindwa kuchochea mabadiliko haramu ya kiutawala nchini Zimbabwe.