Tanzania yasisitiza kuunga mkono kithabiti sera ya kuwepo kwa China Moja
2022-08-05 09:18:58| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania jana ilitangaza taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisema Tanzania inashikilia kanuni na makubaliano ya mawasiliano kati ya pande hizo mbili ikiwemo sera ya kuwepo kwa China moja na kuona kuwa Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China na daima inaunga mkono maslahi makuu ya China.