Marekani yatangaza homa ya nyani kuwa hali ya dharura ya afya ya umma
2022-08-05 09:03:30| CRI

Serikali ya Marekani imetangaza ugonjwa wa homa ya nyani kuwa hali ya dharura ya afya ya umma nchini humo, ikiwa ni zaidi ya wiki moja tangu Shirika la Afya Duniani lithibitishe kuwa ugonjwa huo ni hali ya dharura ya kimataifa.

Waziri wa Afya na Huduma za Umma wa Marekani Bw. Xavier Becerra jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa wako tayari kukabiliana na hali katika ngazi inayofuata na kumtaka kila Mmarekani kuuchukulia ugonjwa huo kwa makini zaidi.

Hadi kufikia Alhamisi, Marekani imethibitisha zaidi ya watu 6,600 walioambukizwa homa ya nyani, ambayo ni karibu asilimia 25 ya jumla ya watu 25,800 duniani.