Wiki ya kwanza ya mwezi Agosti ya kila mwaka ni Wiki ya Unyonyeshaji, ambapo mamlaka mbalimbali zinatumia wiki hiyo kueleza umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto. Kauli mbiu ya mwaka huu kwa Wiki hii ni “Chukua Hatua Endeleza Unyonyeshaji: Elimisha na Usaidizi.” Katika maadhimisho ya mwaka huu, Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali za nchi mbalimbali duniani kutenga rasilimali zaidi ili kulinda, kukuza, na kusaidia sera na programu za unyonyeshaji, haswa kwa familia zilizo hatarini zaidi ambazo zinaishi katika mazingira ya dharura.
Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tutazungumzia zaidi umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto, na athari anazopata mtoto kama akikosa maziwa ya mama, lakini pia athari kwa mama anaposhindwa kumyonyesha mtoto wake.