PLA lafanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja yasiyo na kifani kwenye maeneo yanayozunguka kisiwa cha Taiwan
2022-08-05 09:08:57| CRI

Kamandi ya Uwanja wa Vita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) jana ilifanya mazoezi na mafunzo ya pamoja kwenye maeneo yanayozunguka kisiwa cha Taiwan, kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

Kwenye mbinu za kushambulia kwa masafa marefu, roketi mpya zilirushwa na kamandi ya jeshi la kivita, likipiga sehemu zilizolengwa kwa usahihi kabisa katika eneo la mashariki la mlango bahari wa Taiwan, na kufikia matokeo yaliyokuwa yanatakiwa. Samabmba na mbinu hizo, pia mashambulizi yalihusisha aina mbalimbali za makombora ya kawaida yaliyorushwa kwa roketi, na kulenga maeneo yaliyokusudiwa ya mashariki ya kisiwa cha Taiwan. Uwezo wa kikosi wa kurusha kwa usahihi pia uliangaliwa.

Liu Dongkun, afisa mwandamizi wa kamandi ya uwanja wa vita ya mashariki, amesema vikosi vyote vimeonesha ujasiri na moyo wao wa mapambano usioshindikana. Akiongeza kuwa vikosi vitakamilisha kazi waliyokabidhiwa na chama na watu wa China, na kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi.