Kundi la Jihad latangaza kufikia makubaliano ya kusimamisha mapambanao na Israel
2022-08-08 10:01:03| cri

Kundi la Jihad la Palestina jana limetoa taarifa likitangaza kuwa, chini ya usuluhishi wa Misri, limefikia makubaliano ya kusimamisha mapambano kati yake na Israel.

Katika makubaliano hayo, Misri imeahidi kufanya juhudi za kuishawishi Isarel kuwaachilia mateka wawili wa kundi la Jihad.

Makubaliano hayo yameanza kutekelezwa kuanzia saa tano na nusu jana kwa saa za huko.