Sudan yamwita balozi wa Chad kutokana na tuhuma za shambulizi la kuvuka mpaka
2022-08-08 08:56:59| CRI

Sudan imemwita balozi wa Chad nchini humo Jumamosi ili kupinga shambulizi la kuvuka mpaka wa nchi lililofanywa na makundi yenye silaha ya Chad, ambapo raia takriban 18 wa Sudan waliuawa.

Shirika la habari la Sudan (SUNA), limesema kaimu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali Al-Sadiq ameitaka Chad kuwakamata washambuliaji na kurejesha mamia ya ngamia walioibiwa haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake, balozi wa Chad amesema nchi yake itafanya juhudi zote kudumisha na kukuza uhusiano na Sudan kwa njia inayolinda usalama, amani na utulivu, na haitaruhusu jambo lolote linaloweza kuvuruga uhusiano huo.