Rais wa Marekani aidhinisha msaada mkubwa wa silaha kwa Ukraine
2022-08-09 08:41:38| cri

Rais wa Marekani Joe Biden jana alitangaza kuwa nchi hiyo itaipatia Ukraine msaada wa nyongeza  wa usalama wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1, ikiwa ni silaha nyingi zaidi kutolewa kwa mara moja tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Tangu rais Biden aingie madarakani, msaada ulioahadiwa kutolewa na  Marekani kwa  usalama  wa Ukraine umefikia dola za kimarekani bilioni 9.8 kwa jumla.