Mabalozi wa nchi za kiislamu nchini China wasifu sera za China katika kushughulikia masuala ya mkoa wa Xinjiang
2022-08-09 08:34:48| CRI

Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi 30 za kiislamu nchini China walitembelea mkoa wa Xinjiang kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi huu.

Mabalozi hao wamesifu sera za serikali ya China katika kushughulikia masuala ya mkoa wa Xinjiang kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa wananchi, na  wakisifu juhudi kubwa zilizofanywa na mafanikio mazuri yaliyopatikana mkoani Xinjiang katika maendeleo ya uchumi na mshikamano wa makabila.

Hayo yalisemwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin wakati akijulisha safari ya mabalozi hao kwenye mkoa wa Xinjiang.

Wang Wenbin amesema, wakati wa safari hiyo, mabalozi hao walijionea  hali halisi kuhusu masikilizano kati ya makabila mbalimbali, uhuru wa kuabudu, na mafanikio yaliyopatikana katika kuondoa  umaskini na kuleta ustawi wa vijiji katika mkoani Xinjiang.