Watu mashuhuri wa Afrika: “Mtego wa Madeni” unaosisitizwa na nchi za Magharibi ni kauli potoshi
2022-08-11 14:13:35| CRI

Ni wakati mwingine tena tunapokutana katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing. Ni kipindi ambacho kinaelezea masuala kadha wa kadha kuhusu ushirikiano na uhusiano kati ya nchi za Afrika na China.

Miongoni mwa mambo tuliyokuandalia katika kipindi cha leo ni pamoja na habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, pia tutakuwa na ripoti inayoelezea maoni ya wataalamu na watu mashuhuri wa Afrika kwamba “Mtego wa Madeni” unaosisitizwa na nchi za Magharibi ni kauli potoshi, lakini pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yanayozungumzia Kenya kutarajia fedha zaidi za kigeni kwa kuuza parachichi kwenye soko la China.