Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais laendelea nchini Kenya
2022-08-11 08:33:18| CRI

Zoezi la kuhesabu na kuhakiki kura katika uchaguzi mkuu wa Kenya limeanza kufanyika baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.

Jumanne jioni, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) Wafula Chebukati alisema, zoezi la kupiga kura lilikamilika katika vituo vyote nchini humo na kazi ya kuhesabu kura imeanza kufanyika.

Amesema zoezi la kuhesabu kura linafanyika katika ngazi tatu, yaani  ngazi ya vituo vya kura,  ya majimbo na ya kitaifa, na kuongeza kuwa, katika kuhakiki hesabu kwenye  ngazi ya kitaifa, wanahakiki picha za fomu zilizotumika katika kupata matokeo.