Kampuni za China kuendeleza eneo jipya la viwanda nchini Ethiopia
2022-08-12 08:48:44| CRI

Tume ya Uwekezaji nchini Ethiopia (EIC) imesaini makubaliano na kampuni ya Chuma ya WODA ya China na wenzi wake ili kujenga eneo la viwanda nchini Ethiopia.

Makubaliano hayo yanahusisha kufanyia maboresho kampuni ya Chuma ya WODA kuwa Eneo la Viwanda yla WODA ikiwa na uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 95 katika mji wa Sebeta pembezoni mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Naibu mkuu wa EIC Daniel Teressa ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua baada ya hafla ya kusaini makubaliano hayo kuwa,  Eneo la Viwanda la  WODA itakuwa na mchango muhimu katika kutoa nafasi za ajira, kukarabati msingi wa viwanda na kuwa chanzo muhimu cha fedha za kigeni zinazohitajika sana nchini Ethiopia.