China ni nchi kubwa zaidi ya G20 kwa kusitisha ulipaji wa madeni
2022-08-12 08:50:15| cri


 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema, hivi karibuni viongozi wa Bangladesh akiwemo waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo waliishukuru China kwa kutoa misaada na mikopo kwa nchi yao.

Wang Wenbin amesema, China inafuatilia sana tatizo la nchi zinazoendelea la kulipa madeni, na inatekeleza kihalisi pendekezo la Kundi la Nchi 20 (G20) kuhusu kusitisha ulipaji wa madeni, na China imekuwa ni nchi iliyotoa muda mrefu zaidi wa ulipaji wa madeni katika kundi hilo.