Wasomi zaidi ya 70 waitaka serikali ya Marekani kurejesha mali za Benki Kuu ya Afghanistan
2022-08-12 08:49:47| CRI

Wanauchumi na wasomi zaidi ya 70 wameandika barua ya wazi kwa rais wa Marekani Joe Biden na waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen, wakiitaka serikali ya Marekani irejeshe mara moja dola za kimarekani bilioni saba za Benki Kuu ya Afghanistan ambazo zilihifadhiwa na Marekani.

Barua hii iliandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Uchumi na Sera cha Marekani, na wasomi waliosaini majina yao kwenye barua hiyo wanatoka kote duniani, akiwemo mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Uchumi Joseph Stiglitz.

Katika barua hiyo, wasomi hao wanaonesha wasiwasi mkubwa juu ya migogoro ya kiuchumi na kibinadamu inayoendelea nchini Afghanistan, haswa sera za Marekani zinazochochea migogoro hiyo.