Maonesho ya kimataifa ya njia ya hariri yahimiza ushirikiano wa kina wa “Ukanda mmoja, Njia moja”
2022-08-15 08:54:59| CRI

Maonesho ya sita ya kimataifa ya Njia ya Hariri yamefunguliwa mjini Xi’an, Mkoani Shaanxi, ajenda kuu ikiwa ni kuhimiza ushirikiano kati ya nchi zilizo kwenye eneo la ukanda huo.

Yakiwa na kauli mbiu ya kuhimiza muunganiko na mafungamano kwa ajili ya maendeleo ya pamoja, maonesho hayo yamevutia washiriki kutoka zaidi ya nchi 70, ikiwa ni pamoja na Korea Kusini, Thailand na Singapore, huku Uzbekistan ikiwa ni mgeni wa heshima.

Pendekezo la “Ukanda mmoja, Njia moja” lilitolewa na China mwaka 2013, kwa lengo la kujenga mtandao wa biashara na miundombinu inayounganisha bara la Asia na Ulaya, na maeneo mengine ya kando ya njia hiyo ya kale ili kuleta maendeleo ya pamoja.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana China ilikuwa imejenga maeneo 79 ya ushirikiano wa uchumi na biashara kwenye nchi 24 kwenye ukanda huo, imewekeza dola za kimarekani bilioni 43 na kuzalisha ajira laki 3.46.