Msomi wa Nigeria: Kucheza “karata ya Taiwan” kunaharibu sifa ya kimataifa ya Marekani
2022-08-15 08:32:42| CRI

Waraka uliotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mambo ya Taiwan na Ofisi ya Habari katika Baraza la Serikali la China umefuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Mkurugenzi na Taasisi ya Utafiti wa China ya Nigeria Bw. Charles Onunaiju alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) amesema ukweli wa Taiwan kuwa sehemu ya China tangu zama za kale una ushahidi thabiti wa kihistoria na kisheria, na kanuni ya kuwepo China moja duniani ni makubaliano ya jumla ya jumuiya ya kimataifa yaliyothibitishwa na azimio la Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Bw. Onunaiju amesema, Taarifa ya Kuanzishwa kwa Uhusiano wa Kibalozi kati ya China na Marekani imetangaza wazi kuwa serikali ya Marekani inatambua msimamo wa China, yaani kuwepo kwa China Moja duniani, na Taiwan ni sehemu ya China. Lakini katika muda mrefu uliopita, kwa upande mmoja Marekani inasisitiza kufuata sera ya China Moja, lakini kwa upande mwingine inacheza “karata ya Taiwan” na kuingilia mambo ya ndani ya China. Bw. Onunaiju anaona, kucheza “karata ya Taiwan” kumekuwa ni ujanja wa kawaida wa wanasiasa wa Marekani, hasa katika wakati ambapo uchaguzi unakaribia.

Bw. Onunaiju amesema, safari ya kiuchokozi ya Spika wa Baraza la Chini la Bunge la Marekani Bibi Nancy Pelosi kisiwani Taiwan imetikisa vibaya msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani, na kuzusha wasiwasi mpya wa dunia kuhusu mwelekeo wa uhusiano huo. Amesema, karibu nchi zote duniani zinafuata kwa makini kanuni ya China Moja, tabia ya "sura mbili" ya Marekani kuhusu suala la Taiwan si kama tu imetengwa na jumuiya ya kimataifa, lakini pia imeharibu sifa ya kimataifa ya Marekani yenyewe.

Bw. Onunaiju ameongeza kuwa sera ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili” ambayo ni mpango muhimu wa kitaasisi uliotolewa na China ili kutimiza muungano kwa njia ya amani, imezingatia kikamilifu suala la uwepo wa mifumo tofauti katika kando mbili za mlango bahari wa Taiwan, na ni mchango muhimu kwa amani ya dunia. Wakati huohuo, China pia haiahidi kutotumia nguvu dhidi ya uingiliaji wa nje na wafarakanishaji wachache wanaotaka kuitenga Taiwan kutoka China pamoja na shughuli zao haramu, Bw. Onunaiju anaona hili ni jibu la kimantiki la nchi yoyote huru wakati mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake vinatishiwa.