Rais wa China atoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kujenga ushirikiano wa maendeleo ya dunia
2022-08-15 08:44:31| CRI

Rais Xi Jinping wa China alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufikia makubaliano ya kuhimiza maendeleo, kuweka mazingira wezeshi na kuhimiza nguvu mpya ya maendeleo ya kimataifa kufanya kazi kwa pamoja kwa ubia wa maendeleo wa kimataifa.

Rais Xi aliyasema hayo kwenye barua ya pongezi kwa mkutano wa Kimataifa wa mshikamano wa jumuiya za Kiraia kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Dunia.


Habari nyingine zinasema Rais Xi Jinping wa China Jumamosi alijibu barua kutoka Li Peisheng na Hu Xiaochun, wanaosifiwa kuwa “Wasamaria Wema wa China”, ambao wanafanya kazi kwenye eneo la utalii la Mlima Huangshan katika mkoa wa mashariki wa Anhui, akieleza matumaini yake kuwa wataendelea na kazi zao kama mifano ya kuigwa.

Kwenye barua yake Rais Xi amesisitiza kuwa umuhimu wa “Wasamaria Wema wa China” ni kwamba wafanyakazi hawa wa mashinani wamepata mafanikio yasiyo ya kawaida kwenye kazi zao za kawaida. Ameeleza matumaini yake kuwa wataendelea kuweka mifano ya kuigwa ili kutoa ushawishi chanya, kuwahamaisha watu walio karibu nao kufanya chochote wanachoweza kwa manufaa ya jamii na kuhimiza maadili makuu ya kijamaa. Rais Xi pia anatumai kuwa watawahamasisha watu walio karibu nao kuwa raia wema, wafanyakazi wazuri na wanafamilia wazuri, na kuchangia mchakato wa ustawishaji mkubwa wa taifa la China.