Shirika la ndege la Tanzania kuanzisha usafiri wa ndege wa kwenda Nigeria na Ghana
2022-08-16 08:57:02| CRI

Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) linapanga kuanzisha  usafiri wa ndege za kwenda Nigeria na Ghana mwaka kesho katika juhudi zake za kupanua biashara yake barani Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa ATCL Bw. Ladislaus Matindi ameeleza kuwa shirika hilo linapanga kuhimiza huduma za ndani huku pia likianzisha  usafiri mpya wa ndege wa kwenda sehemu nyingine barani Afrika na duniani. Amesema kuwa sasa usafiri wa ndege wa kwenda Afrika Kusini na China zimerejeshwa baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na janga la COVID-19, na usafiri wa ndege wa  kwenda miji ya Goma na Kinshasa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) pia unatarajiwa kuanzishwa.