China yahimiza utekelezaji kamili wa makubaliano ya kusimamisha vita nchini Yemen
2022-08-16 08:23:17| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun, ametoa wito wa kutekelezwa kikamilifu kwa makubaliano ya kusimamisha vita nchini Yemen, kupanua mafanikio yaliyopatikana na kuweka umakini katika kuboresha hali ya kibinadamu nchini humo.

Akitoa hotuba kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Yemen, Balozi Zhang Jun amesema, idadi ya vifo vya raia vilivyosababishwa na operesheni za kijeshi imepungua kwa kiasi kikubwa tangu  usimamishaji vita ulipoanza kutelekezwa.

Balozi Zhang amezitaka pande husika nchini Yemen kutekeleza kikamilifu ahadi ya kusimamisha  mapambano, kuepuka mashambulizi yote dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia, kutumia ipasavyo utaratibu wa kamati ya uratibu wa kijeshi wa kudumisha mawasiliano ya kawaida, na kutatua masuala yaliyopo kwa njia ya mazungumzo.