Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan yaongezeka hadi 75
2022-08-17 08:42:46| CRI

Baraza la ulinzi wa raia la Sudan limesema idadi ya vifo vilivyosababishwa na mvua na mafuriko nchini humo imeongezeka hadi 75 huku watu wengine 30 wakiwa wamejeruhiwa. Licha ya hayo, kutokana na tangazo lililotolewa na baraza hilo, nyumba 12,551 zimebomoka na nyingine 20,751 zimeharibiwa kutokana na maafa hayo.

Ripoti iliyotolewa Jumapili iliyopita na Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema watu takriban elfu 38 nchini Sudan wameathiriwa na mvua na mafuriko tangu kuanza kwa msimu huu wa mvua.