Magaidi 13 wa al-Shabaab wauawa kwenye shambulizi la anga Somalia
2022-08-18 08:23:12| CRI

Jeshi la Somalia limewaua wapiganaji 13 wa kundi la al-Shabaab kwenye shambulizi la anga lililofanyika karibu na wilaya ya Teedaan, katikati ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Taifa la Somalia (SNA), shambulizi hilo la anga lilifanywa Jumapili pamoja na Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (Africom), na liliwalenga magaidi ambao walikuwa wakishambulia vikosi vya jeshi la Somalia SNA kwenye eneo la mbali karibu na Teedaan.

Jeshi la Somalia na Africom wameapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya kundi la al-Shabaab ili kuepusha vifo vya raia wasio na hatia.