Serikali ya Msumbiji yapunguza masharti ya viza ili kuvutia uwekezaji na utalii
2022-08-18 08:32:45| CRI

Serikali ya Msumbiji imetangaza hatua kadhaa za kisera kuhusu viza na muda wa wageni kuwepo Msumbiji kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia watalii na wawekezaji.

Msemaji wa serikali ya Msumbiji Bw Filimao Sauze amesema mabadiliko hayo ni sehemu ya hatua 20 za “kuchochea uchumi” zilizotangazwa wiki iliyopita na Rais Filipe Nyusi.

Bw Suaze amesema hatua hizo ni pamoja na mageuzi ya kimuundo yatakayoifanya Msumbiji iwe eneo linalovutia wawekezaji, kuweka mkazo kwenye kuboresha mazingira ya biashara na kutengeneza nafasi za ajira, na kutoa kipaumbele kwa sekta binafsi kwenye mageuzi ya kiuchumi na maendeleo.

Kupitia mpango huo, utaratibu wa kutoa viza kwa njia ya kielektroniki utaanzishwa, na viza itatolewa ndani ya siku tano.