Kampuni iliyowekezwa na China kujitahidi kuisaidia Botswana kupunguza uagizaji wa saruji
2022-08-18 08:32:08| CRI

Kampuni ya Cheetah Cement iliyowekezwa na China katika mji wa Francistown nchini Botswana, imesema itajitahidi kutoa mchango mkubwa kuhakikisha Botswana inafikia hali ya kutoagiza saruji kutoka nje.

Meneja wa kampuni hiyo Bw. Hui Ming, amesema kwa sasa Botswana inahitaji saruji tani laki 6.2 kwa mwaka, ambazo kabla ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo ilikuwa inategemea sana kuagiza kutoka nje. Amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka kesho wanatarajia uzalishaji utafikia tani laki 9, na ziada inatarajiwa kuuzwa katika nchi jirani ikiwemo Zimbabwe. 

Mkuu wa Kituo cha uwekezaji na biashara cha Botswana Bw. Keletsositse Olebile, amesema kama Botswana ikizalisha saruji yake yenyewe, itaokoa zaidi ya dola milioni 90 za kimarekani kwa mwaka.