China yaihimiza Marekani kufuata kwa makini kanuni ya China moja
2022-08-18 08:22:36| CRI

China imeihimiza Marekani kujifunza kutokana na historia, kuheshimu taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani na kufuata kwa makini kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin aliyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari alipoulizwa kuhusu maadhimisho ya miaka 40 ya Taarifa ya Agosti 17, ambayo ni moja ya taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani.

Bw. Wang amesema Taarifa ya Agosti 17, Taarifa ya Shanghai na Taarifa ya Pamoja kuhusu Kuanzishwa kwa Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Marekani, ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambao kiini chake ni kanuni ya kuwepo kwa China Moja.