Kuavya mimba kuna athari gani kwa afya ya uzazi kwa mwanamke?
2022-08-19 08:41:21| CRI

Hivi karibuni mjadala mkali umezuka nchini Marekani kuhusu haki ya kuavya mimba. Baadhi ya Wamarekani wanafurahia sheria ya uhuru wa kuavya mimba, huku wengine wakipinga sheria hiyo, wakisema baadhi ya wanawake wataitumia vibaya ili kutimiza mahitaji yao. Baadhi ya wanawake walioandamana hivi karibuni nchini Marekani walisema, walishiriki maandamano hayo kwa kuwa wanaamini kuwa wanawake wanapaswa kuwa na sauti na uamuzi juu ya miili yao, na kwamba suala hilo ni haki ya msingi ya binadamu. Lakini swali ni kwamba, kuavya mimba kuna athari gani kwa afya ya uzazi kwa mwanamke? Kipindi cha Ukumbi wa Wanawake leo hii kitazungumzia suala hilo pamoja na mengine yanayohusiana na afya ya uzazi kwa mwanamke.