Tanzania yatangaza mapumziko ya kitaifa katika siku ya sensa 2022
2022-08-19 09:11:32| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameamua tarehe 23 mwezi huu kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kuruhusu sensa ya watu na makazi kufanyika.

Taarifa hiyo imetolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Kassim Majaliwa wakati akihutubia mkutano wa 7 wa Kamati ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi uliofanyika mjini Dar es Salaam. Bw. Majaliwa amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya kuwezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika sensa hiyo wakiwa na nafasi ya kukaa nyumbani.

Rais Samia alitangaza tarehe ya kufanyika kwa sensa hiyo mwezi wa Aprili mwaka huu, akihamasisha raia kushiriki vizuri kwenye kazi hiyo, ili kusaidia serikali kuweka mipango ya kutoa huduma mbalimbali kwa watu wake.