Wizara ya Mambo ya Nje ya China yakanusha kauli mbaya zilizotolewa na balozi wa Marekani nchini China kuhusu Taiwan
2022-08-23 09:41:45| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imekanusha kauli zisizo sahihi za balozi wa Marekani nchini China Nicholas Burns, kuhusu kisiwa cha Taiwan, akisema kauli zake zinachanganya ukweli na uongo, na kwa mara nyingine tena zinapotosha na kuonesha mantiki ya umwamba wa Marekani.

Agosti 19, Burns kwenye mahojiano yake na CNN alisema China imeikuza kupita kiasi ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi kisiwani Taiwan, na sasa imekuwa wakala anayechangia hali isiyo na utlivu kwenye mlango bahari wa Taiwan na kusababisha mgogoro katika uhusiano wa Marekani na China. Pia alitaja kuhusu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Xie Feng kumuita baada ya ndege iliyombeba Pelosi kutua huko Taiwan, akieleza kwamba mkutano wao ulikuwa na “malumbano”.

Ikijibu kuhusu kauli za Burns, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kabla ya ziara ya uchokozi ya Pelosi kisiwani Taiwan, China iliionya mara nyingi Marekani, ikiiambia madhara makubwa ya ziara hiyo na kuweka wazi kwamba matatizo yote yatakayotokea baada ya ziara yatabebwa na Marekani. Pia amesema itakuwa sio haki kusema kwamba Marekani haikuonywa juu ya matokeo ya ziara ya Pelosi.