UM waonya ukame utasababisha utapiamlo mkali katika maeneo ya Pembe ya Afrika na Sahel
2022-08-24 09:34:15| CRI

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeonya kuwa zaidi ya watoto milioni 2.8 katika eneo la Pembe ya Afrika na Sahel tayari wanataabika na utapiamlo mkali na wengi wanaweza kufa kama msaada wa dharura hautatolewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russel amesema watoto hao wapo kwenye hatari ya kufa kutokana na magonjwa yanayotokana na maji kuliko wale wenye lishe bora kwani utapiamlo mkali na magonjwa yanayotokana na maji yanakinzana. Aidha amefafanua kuwa familia za maeneo yaliyoathirika na ukame zinalazimika kuwa na machaguo yasiyowezakana.

Amesisitiza kuwa njia pekee ya kuzuia msukosuko huu ni kwa serikali, wachangiaji, na jamii ya kimataifa kujitokeza kufadhili ili kuwafikia watoto wenye mahitaji zaidi, na kutoa msaada wa muda mrefu ambao ni nyumbufu ili kufanya msukosuko huo usijirejee tena.