Marekani yatangaza kuipatia Ukraine msaada wa silaha wenye thamani ya dola bilioni tatu
2022-08-25 09:32:23| CRI

Marekani imetangaza kuipatia Ukraine msaada wa ziada wa usalama, wenye thamani ya dola takriban bilioni tatu za kimarekani, ambao ni msaada mkubwa zaidi wa silaha kupatiwa Ukraine tangu mapambano kati ya Russia na Ukraine yalipoanza nusu mwaka uliopita.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ilitoa taarifa ikisema silaha hizo zitatolewa kwa mujibu wa makubaliano na makampuni ya kutengeneza silaha, ambapo wizara ya ulinzi itanunua silaha hizo kwa kutumia fedha zilizoidhinishwa na bunge la Marekani kwa ajili ya mpango wa msaada wa usalama kwa Ukraine.

Tangu Biden alipoingia madarakani, Marekani imeahidi kuipatia Ukraine msaada wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 13.5 za kimarekani.