Rais Xi atoa barua ya pongezi kwa kongamano la 5 la ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya China na Afrika
2022-08-25 18:46:31| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa pongezi kwa kongamano la 5 la ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya China na Afrika, lililofunguliwa leo hapa Beijing.

Rais Xi amesema China na nchi za Afrika zina muskabali wa pamoja, vyombo vya habari vya pande hizi mbili vinabeba majukumu makubwa katika kuzidisha ushirikiano wa kuaminiana, kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo duniani.

Rais Xi amesema katika miaka 10 iliyopita tangu kongamano hilo lianzishwe, vyombo vya habari vya China na Afrika vimetoa jukwaa muhimu la kuongeza mawasiliano na ushirikiano wa pande mbili, kuhimiza mawasiliano na kufundishana kati ya tamaduni za pande mbili, na kuimarisha uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika.

Rais Xi amesema ni matumaini yake kuwa vyombo vya habari vya pande hizo mbili vitachangia kuelezea vizuri uhusiano kati ya China na Afrika katika zama mpya, na kusukuma mbele mustakbali wa pamoja wa binadamu.