Rais Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kusini wapongezana kwa kutimiza miaka 30 ya uhusiano wa kidiplomasia
2022-08-25 09:24:43| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wamepeana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye salamu zake, Rais Xi alidokeza kuwa China na Korea Kusini ni majirani wa kudumu wanaoangaliana katika kando mbili za bahari, na watu wa nchi hizo wanafurahia historia ndefu ya kirafiki. Tangu China na Korea Kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 30 iliyopita, kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano wa nchi hizo umekuwa ukiendana na wakati, umeendelezwa kwa njia zote na kuzaa matunda, jambo ambalo limeleta manufaa makubwa kwa nchi hizo mbili na watu wake, na pia kutoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya kikanda na dunia.

Kwa upande wake, Rais Yoon Suk-yeol wa Korea Kusini amebainisha kuwa Korea Kusini na China ziko karibu kijiografia na zinafurahia uhusiano wa muda mrefu wa kihistoria na kiutamaduni, na kusema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1992, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja kama vile siasa, uchumi na utamaduni umeshuhudia maendeleo makubwa na ya kimkakati, na uhusiano wa pande hizi mbili umeendelea kuimarishwa.