Rais Xi atoa barua ya pongezi kwa Baraza la 5 la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika
2022-08-26 09:42:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa pongezi kwa  Baraza la 5 la ushirikiano wa vyombo vya  habari kati ya China na Afrika, lililofunguliwa tarehe 25 hapa Beijing.

Rais Xi amesema China na nchi za Afrika zina muskabali wa pamoja, vyombo vya habari vya pande hizi mbili vinabeba majukumu makubwa katika  kuimarisha hali ya kuaminiana na ushirikiano, kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo duniani.

Rais Xi amesema katika miaka 10 iliyopita tangu  baraza hilo lianzishwe, vyombo vya habari vya China na Afrika vimetoa jukwaa muhimu la kuongeza mawasiliano na ushirikiano  kati ya pande mbili, na kufanya kazi muhimu kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano na kufundishana kati ya pande mbili   katika sekta ya utamaduni , na kuimarisha uhusiano wa  wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika.

Rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa vyombo vya habari vya pande hizo mbili vitachangia  kusimulia vizuri hadithi kuhusu China na Afrika katika zama mpya, kueneza maadili ya pamoja ya binadamu  na kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.