WHO lazindua mpango wa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona nchini Somalia
2022-08-26 09:46:19| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limezindua mpango mpya wa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona kwenye jamii nchini Somalia.

Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Bw. Mamunur Rahman Malik jana alisema mpango huo utaondoa mianya iliyopo Somalia katika masuala ya uratibu, usimamizi, utoaji wa chanjo na operesheni ya kukabiliana na janga la Corona, na kusaidia kurejesha mfumo wa afya wa nchi hiyo na kuufanya uwe shirikishi na wenye usawa zaidi.

Akitoa taarifa mjini Mogadishu Malik amesema WHO ikishirikiana na wenzi wake ikiwemo serikali ya Somalia, watachukua hatua zaidi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. Ameongeza kuwa hatua hiyo itazuia kuibuka tena kwa mlipuko wa virusi, na kupunguza zaidi athari mbaya za janga hilo kwenye huduma nyingine za matibabu.