Watu zaidi ya elfu moja wafariki kutokana na mvua kubwa nchini Pakistan
2022-08-29 08:55:03| CRI

Idara ya usimamizi wa maafa ya Pakistan imesema, watu 1,033 wameuawa na wengine 1,527 kujeruhiwa tangu katikati ya mwezi wa Juni kutokana na maafa mbalimbali yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na idara hiyo, mvua hiyo pia ilisababisha nyumba kadhaa kubomoka, vifo vya mifugo na uharibifu wa madaraja na barabara.