Mkutano wa Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia washindwa kufikia maoni ya pamoja kuhusu nyaraka za matokeo
2022-08-29 08:52:10| cri


 

Mkutano wa 10 wa kukagua na kujadili Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa umemalizika ijumaa iliyopita, na kushindwa kufikia maoni ya pamoja kuhusu nyaraka za matokeo baada ya mwezi mmoja.

Mkurugenzi wa Ofisi ya udhibiti wa silaha ya China ambaye pia ni mwakilishi wa China kwenye suala la kupunguza silaha Bw. Fu Cong alisema, ingawa mkutano huo haukufikia makubaliano ya mwisho, lakini pande mbalimbali zilijaribu kutafuta maoni ya pamoja kuhusu masuala yenye utatanishi, ikimaanisha umuhimu wa kutafuta njia ya kukabiliana na changamoto za mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia.