Rais wa Iran asema ni lazima kutatua suala la uhakikishaji wa nyukilia
2022-08-30 08:34:26| cri


 

Rais Seyed Ebrahim Raisi wa Iran jana amesema, ni lazima kwanza kutatua suala la uhakikishaji wa nyuklia, ili kufikia makubaliano katika mazungumzo kuhusu kurejesha utendaji wa Makubaliano ya suala la nyuklia la Iran.

Rais Raisi amesema, kama suala la uhakikishaji wa nyuklia halitatatuliwa, hakutakuwa na matokeo yoyote hata kama makubaliano yatafikiwa. Amesema Iran haijawahi kujitoa kwenye meza ya mazungumzo, na ni lazima kwa Marekani kuondoa vikwazo dhidi yake, na nchi zilizokiuka makubaliano ya suala la nyuklia la Iran lazima zitekeleze ahadi zao tena.