Mkutano wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China kufanyika tarehe 16 Oktoba
2022-08-31 12:44:40| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana imeitisha mkutano kuhusu kazi za maandalizi za Mkutano wa 20 wa Wajumbe Wote wa CPC.

Mkutano huo umeamua kuwa Mkutano wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China utafanyika tarehe 16 Oktoba mjini Beijing.