Watu zaidi ya 12 wauawa katika mapigano nchini Iraq
2022-08-31 08:45:27| cri

Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq imesema, watu zaidi ya 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika jumatatu katika eneo la "Ukanda wa Kijani" la mji wa Baghdad.

Mapema siku hiyo, kiongozi wa kidini wa dhehebu la Shia nchini humo, Bw. Muqtada al-Sadr alitangaza kupitia mtandao ya kijamii kuwa ameamua kutoingilia masuala ya kisiasa na kustaafu, na kwamba makundi yanayohusiana na "Harakati za Sadr" anayoongoza pia yatafungwa.