Baraza la Usalama la UM latoa wito wa kuimarisha juhudi za kuboresha ujenzi wa uwezo barani Afrika
2022-09-01 08:35:27| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano lilitoa wito kwa washirika wote husika kuchukua hatua za uratibu zaidi, hasa kupitia juhudi zinazoimarishwa ili kuboresha ujenzi wa uwezo katika kuzuia migogoro, kujenga amani na changamoto nyingine barani Afrika.

Katika taarifa ya rais iliyowasilishwa na mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama kwa mwezi Agosti Balozi Zhang Jun, Baraza hilo limetambua haja ya kuongeza uungaji mkono katika kuzijengea uwezo nchi za Afrika kwa njia jumuishi inayoendana na malengo halisi, na kuchukua hatua inayofuata hali halisi ya kila nchi na eneo. 

Baraza hilo pia limesisitiza umuhimu wa kuheshimu uongozi wa nchi za Afrika, na kuunga mkono kuimarisha uwezo wao wa kuboresha utawala wa sheria, kuimarisha mashirika ya kisheria, kujenga utawala, kukuza na kulinda haki za binadamu.