Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu 82 nchini Niger
2022-09-01 08:28:52| cri

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Niger imesema, watu 82 wamefariki na wengine 102 kujeruhiwa tangu mwezi Juni kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo pia imesema, watu zaidi ya 110,000 wameathiriwa na mvua hiyo, na mikoa mitatu ya kusini mwa Niger, Maradi, Zinder na Tawa, ndio imeathirika zaidi.