“Miradi Tisa” yahimiza maendeleo ya pande zote ya ushirikiano wa Afrika na China
2022-09-01 10:33:52| CRI

Naibu mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Monique Nsanzabaganwa amesema “Miradi Tisa” iliyotolewa mwaka jana kwenye Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) inawiana sana na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, na itahimiza maendeleo ya pande zote ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.  

Nsanzabaganwa amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua. Amesema miradi hiyo inaendana na mwelekeo wa maendeleo ya kipaumbele, sekta maalum zilizotajwa katika Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, na miradi hiyo inatiliwa maanani sana na pande zote mbili. Amesisitiza kuwa “Miradi Tisa” ni mpango unaozingatia watu kihalisi.

Nsanzabaganwa akitoa mfano wa ushirikiano wa afya, amesema Afrika na China zimepata mafanikio ya ajabu katika kukabiliana na janga la UVIKO-19 kwa mshikamano. Ugonjwa huo ulipotokea barani Afrika, China ilianza kutoa msaada na kuendelea kuzisaidia nchi za Afrika, na pia kuzisaidia kuongeza uwezo wao wenyewe wa kupambana na ugonjwa huo, ikiwemo kuzalisha dawa, vifaa vya matibabu na chanjo. Alipozungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Afrika CDC utakaokamilika Addis Ababa mwishoni mwa mwaka huu, Nsanzabaganwa aamesema anaamini kuwa mradi huu unadhihirisha kikamilifu urafiki kati ya Afrika na China, na pia ni thibitisho wazi la China kutimiza ahadi yake ya kuisaidia Afrika katika sekta ya afya.

Kwa maoni ya Nsanzabaganwa, ushirikiano wa kilimo na kupunguza umaskini pia umepewa kipaumbele katika “Miradi Tisa”. Ametaja kuwa Umoja wa Afrika na China zilitia saini makubaliano ya kuendeleza haraka uzalishaji wa kilimo na chakula wa Umoja huo. Amesema hivi leo dunia inakabiliwa na hatari inayoweza kutokea ya kukatika kwa usambazaji wa chakula na usambazaji wa chakula usio na uwiano, na Umoja wa Afrika unatarajia sana kuendeleza ushirikiano wa kilimo kati ya Afrika na China.

Nsanzabaganwa pia ameipongeza China katika kupunguza umaskini. Amesema katika kupunguza umaskini na kuhimiza maendeleo, mafanikio ya China yametia moyo nchi za Afrika, na nchi za Afrika zinajifunza kutoka kwa China katika kupunguza umaskini ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Ameongeza kuwa kwa kujifunza uzoefu wa China, nchi za Afrika zimepata mafanikio makubwa katika kilimo, biashara ndogo na za kati, uchumi wa kidigitali na nyanja nyingine.

Nsanzabaganwa anaamini kwamba uungaji mkono wa China katika ujenzi wa eneo la biashara huria barani Afrika si kama tu utakuza ushirikiano kati ya China na Afrika katika biashara, uwekezaji na sekta za viwanda.

Licha ya ushirikiano kufuatia FOCAC, mwaka huu, Umoja wa Afrika na China pia zitatia saini makubaliano kuhusu kuanzisha uratibu wa ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Kwa maoni ya Nsanzabaganwa, ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” utasaidia kufikia malengo makuu ya Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, hasa katika ujenzi wa miundombinu.

Nsanzabaganwa amesema Umoja wa Afrika inajitahidi kutimiza umoja halisi wa nchi za Afrika, na mpango huu unahitaji sana uwekezaji. Huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Umoja huo, washirika ikiwa ni pamoja na China, wanakaribishwa kuwekeza barani Afrika ili kuisaidia kusonga mbele zaidi.