Wanaanga wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 wakamilisha shughuli za kwanza za nje
2022-09-02 09:43:24| cri


 

Shirika la Anga Za Juu la China (CMSA) limesema mapema leo,  kwamba wanaanga wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 Bw. Chen Dong na Bi. Liu Yang wamekamilisha shughuli zao za nje ya chombo (EVAs), na kurudi kwenye Maabara ya chombo hicho.

Shirika hilo limesema, hii ni mara ya kwanza kwa wanaanga wa China kutekeleza shughuli za nje ya chombo cha anga ya juu kwa kutumia mkono mdogo wa mitambo, na kutangaza kuwa, majukumu ya Ijumaa yamekamilika kwa mafanikio.