Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan yaongezeka hadi 112
2022-09-05 09:26:48| CRI

Baraza la Ulinzi wa Raia la Sudan limesema idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko nchini Sudan imeongezeka hadi kufikia 112, maelfu ya nyumba na mamia ya vifaa vya umma na maduka kuharibiwa.

 Vijiji zaidi ya 250 vya kaskazini, katikati na magharibi mwa nchi hiyo vimekumbwa na mvua kubwa kwa mwezi mmoja. Mwezi uliopita baraza la mawaziri la Sudan lilitangaza hali ya dharura katika majimbo sita yaliyoathiriwa na mafuriko nchini humo yakiwemo River Nile, Gezira, White Nile, West Kordofan, South Darfur na Kassala.

 Ofisi ya Umoja ya Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA, imesema takriban watu laki 1.36 nchini Sudan wameathiriwa na maafa ya mvua kubwa na mafuriko tangu mwezi wa Juni mwaka huu.