Russia kuchukua hatua kali kujibu zuio la viza liliowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya raia wake
2022-09-05 08:45:14| CRI

Msemaji wa Ikulu ya Russia Bw. Dmitry Peskov amesema Russia itachukua hatua kali za kulipiza kisasi endapo Umoja wa Ulaya utaweka rasmi vizuizi vya visa dhidi ya raia wa Russia.

Bw. Peskov amesema Russia inafuatilia kwa karibu uamuzi wa Umoja wa Ulaya, na hatua za kulipiza kisasi kwa uhakika zitazingatia maslahi ya Russia, lakini hakudokeza ni hatua gani zitachukuliwa.

Kabla ya hapo mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walikubaliana kusitisha makubaliano ya kurahisisha utoaji wa viza kati ya nchi hizo na Russia. Uamuzi huo ambao haujapitishwa rasmi, utapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya viza mpya zitakazotolewa kwa raia wa Russia.