China yaongeza juhudi kuongeza ujuzi wa sayansi kwa umma
2022-09-05 08:57:39| CRI

China imetoa mwongozo wa kueneza ujuzi wa sayansi ili kuhimiza uvumbuzi wa kisayansi katika jamii, na kukuchukulia  kuhimiza ujuzi wa kisayansi kuwa kazi ya msingi ya kuhimiza maendeleo yanayoongozwa na uvumbuzi, na kuweka umuhimu sawa kwenye kueneza ujuzi wa sayansi na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia.

Mwongozo huo uliotolewa kwa pamoja na Ofisi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la serikali, umetoa malengo halisi ya kueneza sayansi na teknolojia. 

Kwa mujibu wa mwongozo huo, hadi kufikia mwaka 2025 huduma za umma za kueneza ujuzi wa kisayansi zinatakiwa kuwa zimepanuliwa, watafiti wawe na ushiriki zaidi kwenye kueneza ujuzi wa kisayansi, uwiano wa watu wenye ujuzi wa sayansi katika jamii uwe zaidi ya asilimia 15, na mazingira ya kijamii ya kuthamini sayansi na uvumbuzi yanatakiwa kuwekwa. Na hadi kufikia mwaka 2035, uwiano wa watu wenye ujuzi wa sayansi unatakiwa kufikia asilima 25.