Rais Xi Jinping ataka juhudi zote zifanywe kuwaokoa watu kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Sichuan
2022-09-06 08:58:43| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zote zifanywe kuwaokoa watu na kupunguza idadi ya vifo baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.8 kwenye kipimo cha Richter kutokea mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, akisisitiza kuwa kuokoa maisha ya watu kunatakiwa kuwa kipaumbele.

Rais Xi ametoa agizo hilo baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mchana wa jana jumatatu kutikisa wilaya ya Luding, eneo linalojiendesha la kabila la Watibet la Ganzi mkoani humo.

Mpaka sasa tetemeko hilo la ardhi limesababisha vifo vya watu 46 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa, na kuleta uharibifu kwa miundombinu ya usambazaji wa maji na umeme, uchukuzi na mawasiliano ya simu.