Tanzania yazindua kampeni maalumu ya kunyang’nya silaha haramu
2022-09-06 08:59:40| CRI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania imezindua kampeni maalumu kwa raia waanaomiliki silaha kiharamu kusalimisha silaha zao kwa idara husika ndani ya miezi miwili.

Naibu waziri wa mambo ya nje Bw. Jumanne Sagini amezindua kampeni hiyo mjini Dodoma, akiwahimiza wananchi wanaomiliki silaha bila kibali kuzisalimisha la sivyo watachukuliwa hatua.

Bw. Sagini amesema silaha haramu zinatakiwa kukabidhiwa kwa vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa na maofisa watendaji wa vijiji mwezi Septemba na Oktoba.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, watu waliosalimisha silaha zao kwa hiari hawatashitakiwa, lakini wale watakaokutwa na silaha haramu baada ya kampeni hiyo ya miezi miwili watafikishwa mbele ya sheria.